CRDB Bank: Tatizo ni kubwa

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Nilifungua account benki ya CRDB mwezi wa March 2013. Waliniahidi kunipatia kitabu cha hundi baada ya wiki mbili.


Imebakia saa moja kuingia mwezi wa june 2013 wameshindwa kabisa kunipatia kitabu cha hundi, kila ukiwauliza wanatoa sababu chungu nzima.


Nashindwa kabisa kuelewa hii benki ilipataje tunzo ya super brand, miezi mitatu sasa hakuna mauzo ya vitabu vya hundi.


Ndugu zangu hivi huduma za benki zingine ni chafu kama ilivyo kwa CRDB Bank?


Najuta na kumlaumu aliyenielekeza CRDB, naomba msaada wa benki nyingine yenye mtandao mkubwa nchini niweze kuwasiliana nao.


 
 
Back
Top Bottom