Kichaa cha mbwa (Rabies)

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
KICHAA CHA MBWA


Ugonjwa hatari unaopuuzwa sana hasa katika nchi masikini. Ugonjwa huu pia unatatizo la kutotolewa taarifa kamili. Kwa nchi kama Tanzania ugonjwa huu unaonekana kama kaugonjwa kadogo sana. Unaua zaidi ya kipindupindu, unaua karibu ya HIV. Ugonjwa huu unaua zaidi nguvu kazi maana unaua watoto zaidi.


Ugonjwa huu haupo kabisa nchi nyingi za ulaya. Hata marekani ugonjwa huu hauwapati watu maana wanyama wanachanjwa.


Kuchanja (vaccination) ndiyo njia bora na rahisi ya kuzuia ugonjwa huu. Napenda kuwataarifu Watanzania wenzangu kuchanja mbwa wao pamoja na paka ili tuweze kuzuia huu ugonjwa.


 
 
Back
Top Bottom