Mjasiriamali: Utengenezaji wa mafuta ya mgando (ya kupaka)

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Habari wana JF...

Tujifunze utengeneza wa mafuta ya mgando.


MALIGHAFI

1. MICRO WAX

2. WHITE OIL

3. RANGI

4. PERFUME

5. VIFUNGASHIO


JINSI YA KUTENGENEZA


Weka MICRO WAX kilo 1 kwenye sufuria kisha injika jikoni, ikianza kuyeyuka miminia WHITE OIL lita 2 weka RANGI nusu kijiko cha chai kama utapenda.


Ipua kisha weka PERFUME (MANUKATO) kijiko kimoja cha chakula kama utapenda. Acha yaanze kupoa, yakianza kuwa mazito paki kwenye VIFUNGASHIO. Yakiganda funga vifungashio tumia au kauze.


Asante...

-Queen Chagga


 
 
Back
Top Bottom