Amapiano waachiwe wa Afrika Kusini ndiyo wanaziweza Bongo na Naija wanapiga makelele tu!

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Hizi Amapiano toka zilipo anza kuvuma South Africa na wasanii wengi wa Afrika kuanza kuzifanya Wasauzi wamebaki kuwa watabe wa huu mziki.


Wasanii wengi wa nje ya South Africa wanaofanya na wanao jaribu kufanya Amapiano ni kama wanapiga makelele tu hapa nawazungumzia hasa wabongo na Wapopo.


Amapiano za Wabongo na Wapopo wanazichanganya na mabongfleva na maafrobeat mpaka ladha halisi ya Amapiano ina potea kabisa zinabakia kelele.


Wasauzi wanapiga Amapiano kismooth fulani hivi mpaka unafurahi ukikutana na DJ aliepangilia Amapiano za Kisauzi na mwengine anapiga za kibongo na kipopo utofauti wa ukali wa Amapiano ndiyo utauona.


Ata dance moves za kiamapiano za Wasauzi zipo smooth tofauti na Wabongo na Wapopo maguvu mengi mpaka jasho.


Unaweza taja Amapiano zako kali kutoka kwa wasouth unazo zielewa hapa down ⏬


 
 
Back
Top Bottom