Duru: Utangamano, Amani na Ustawi. Taifa linaelekea wapi?

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Ustawi

Taifa lolote linalotazama Ustawi na maendeleo yake huzingatia utangamano na Amani.


Utangamano '(compatibility) ni uwepo wa pamoja(coexist) licha ya tofauti za Raia katika rangi, Imani, itikadi za siasa na Utamaduni. Amani ni utulivu unaoletwa na uwepo wa maridhiano na haki.

Amani si Ukimya unaoletwa na shinikizo (subdue)


Katika miezi michache kuna hali, matukio na kauli zinazoacha swali, Tanzania kama Taifa, je, tuna utangamano na Amani! Taifa linaelekea wapi katika hali ya mivutano na mishuano iliyopo!


Ni kawaida kwa 'shughuli za tasnia au fani fulani kuwa na lugha zake.

Mfano, utani wa Simba na Yanga una lugha zenye karaha kwa asiye elewa lugha ya mpira.


Utani katika siasa kama kuitana nyumbu au zero brain ni wa kawaida nchini.


Pamoja na hayo utani wa simba na Yanga una mipaka yake. Mwisho wa siku Watani hukaa pamoja na kula, hujumuika kuuguzana, na hushirikiana kuzikana. Ni utani wa mpira usiohusisha ubinadamu


Siasa za vyama vingi hazijawahi kusimama bila matatizo, lakini, matatizo yaliyojitokeza yalishughulikiwa na viongozi. Ni ukweli usio na shaka kwamba kuanzia 2020 siasa zetu zimebadilika kwa ubaya!


Tulimsikia kiongozi mmoja ambaye sasa ni RC akitamka '' Wapinzani wapigwe risasi''

Hivi katibuni tukasikia kiongozi mwingine akisema '' Wapinzani wakipotezwa'' polisi wasiwatafute

Kiongozi mwingine akisema ' Wapo Watanzania wanaodhamiria kubeba vidudu vya maradhi.. ''


Tumesikia gari la kiongozi likichomwa moto, wafuasi wa vyama wakirushiana makonde n. K.

Tumesikia watu kutekwa, kupotezwa n. K. Katika mazingira yanayoashiria siasa.


Katika hali ya kujengeka chuki na kauli za kichochezi zikihamasisha uhasama, tulitegemea sheria zichukue mkondo kwa wahusikam kwa sababu sheria ndiyo msingi wa HAKI inayoleta Amani.


Hata hivyo, vyombo husika katika kusimamia na kutoa HAKI ima vimefumbia macho au KUWA NA makengeza kwa sababu za kisiasa kwa masilahi ya viongozi wa kisiasa na si Taifa kwa upana wake


Hali ni mbaya, makundi ya jamii yanaingia katika mivutano yakiwemo ya Dini bila kutaraji


Viongozi wamejikita kutumia nguvu na vyombo vya Dola kutafuta 'Ukimya'' na si Amani.

Viongozi wanahubiri uwepo wa Amani wakijua fika hilo ni Tunda la HAKI isiyokuwepo


Ni katika mivutano iliyopo vyombo vya Dola vilivyonyooshewa vidole kwa muda mrefu kuhusu matukio mabaya ya utekaji, mauaji na dhulma vimejikuta ''viki watoa shaka kwa ushahidi '' waliohisi vinahusika


Kwa mwendo huu, Taifa linaelekea wapi?


Inaendelea


 
 
Back
Top Bottom