Duru: Waziri Kamwelwe asibezwe, ana hoja ya msingi, asaidiwe kuboresha

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
SHERIA YA LESENI MIAKA 45


Kauli ya waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh Isack Kamwelwe kuhusu umri wa madereva kuendesha malori na vyombo vya abiria imepamba habari za wiki hii


Ni kawaida ya Watanzania kuzungumzia jambo kwa jicho wanalotaka na si lile linaloona ukweli. Waziri Kamwelwe ana hoja ya msingi kabisa katika mjadala unaondelea


Kauli yake imekuja ikiwa imechelewa. Ongezeko la ajali nchini limekuwa tishio kwetu sote


Kila inapotokea ajali njia zinazotumika kuzuia au kupunguza ni za mkato na za kizamani kama ulivyo mfumo wetu wa kutoa leseni, kudhibiti, kusimamia bima na kutafuta chanzo na suluhu


Hoja ya waziri inaonekana kuwa na mapungufu kwa mtazamo wa haraka, lakini wazo analotoa ni muhimu sana katika kudhibiti na kukabiliana na wimbi la ajali nchini


Mitandaoni na kwingineko baadhi yetu hatuangalia kiini cha hoja, tunaangali mapungufu ya hoja. Ieleweke alichosema Mh Waziri si sheria ni kusudio la kupeleka mswada Bungeni


Kwa kuelewa hivyo, ni makosa kuanza kukosoa hoja zake kana kwamba miaka 45 ni sheria tayari au kdhani pendekezo la miaka 45 linatosha kuwa suluhu ya tatizo


Kama miaka 45 pekee ndicho kinachodhaniwa ni tatizo, hoja nzima inapoteza maana


Tatizo la ajali linachangiwa na 'factors' nyingi si umri pekee.


Katika kukabiliana na tatizo umri ni sehemu ya suluhu na si suluhu yenyewe


Ni kwa mtazamo huo, tunaona ipo haja ya kumsaidia Mh Waziri kuboresha hoja yake yenye mantiki na ya msingi sana kuliko kukimbilia kulaani, kumbeza na kudharau alichosema


Kwa uzito wa hoja hii tutakuwa na mabandiko kadhaa kwa lengo la kumsaidia waziri kuboresha hoja kwani tatizo la ajali linatugusa sote na sote tunawajibu wa kulitafutia jawabu


Sehemu ya kwanza inafuata


 
 
Back
Top Bottom