Ilianzia CUF, sasa NCCR. CHADEMA wajiandae

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
MGOGORO WA NCCR

CHADEMA WACHUKUE TAHADHARI


Mgogoro wa CUF ulianza kwa mwenyekiti aliyejiuzulu kutaka kurudi katika kiti chake

Tukio halikuwa la kawaida katika siasa za Tanzania lakini limetokea.


CUF walifanya mambo kwa mazoea wakidhani isingewezekana kisiasa au Kisheria.

Msajili wa vyama alijihusisha sana na mgogoro wa CUF Mahakama nayo ikashirikishwa. Mengine yanabaki historia, ACT ikazaliwa, pamoja na CUF wapo katika kikosi kazi


Chadema walikutana Baraza kuu, Mwenye kiti Mbowe aliionya ofisi ya Msajili iache kuchaonganisha vyama bila kueleza kwa undani aina ya uchonganishi.


Kemeo alilotoa lilidhihirisha jambo ndani ya ofisi ya Msajili dhidi ya chama chake


Kuna mgogoro wa NCCR uliomuondoa Mwenyekiti Mbatia katika uongozi wa Chama

Halmashauri imeongozwa na aliyekuwa mwanachama wa vyama mbali mbali Bw J. Selasin


Ofisi ya Msajili iliwakilishwa na Msajili msaidizi wa vyama Bw. S. Nyahoza


Msajili msaidizi alitoa kauli ''akidi ya mkutano imetimia, atajiridhisha orodha ya Wajumbe ''

Kwamba Msajili msaidizi hakuona tatizo lakini atatafuta ukweli akirudi ofisini!!


Kwa kawaida ukweli hutafutwa kwanza kubaini uwepo au kutokuwepo kwa tatizo!!!


Ofisi za NCCR ''zimekombolewa'' na Vijana wa chama, wametoa kauli kupitia You tube

Vijana ha wamenyooshea mkono Ofisi ya Msajili kwamba ina mkono katika mgogoro


Wameeleza chanzo ni Wajumbe waliokwenda TCD Dodoma bila idhini ya chama

Kwamba kikao cha kamati kuu kiliwajadili na nyaraka zilifikishwa Ofisi ya Msajili Ijumaa


Hii ina maana Ofisi ya Msajili ilitambua uwepo wa tatizo kupitia barua ya Kamati kuu

Vijana wamehoji, iweje Ofisi ya Msajili wa vyama itume mjumbe katika kikao cha Halmashauri ikiwa na barua ya Kamati kuu ipo ofisini mwao?


Wanahoji, kwanini Msajili haikujiridhisha ikiwa katiba imefuatwa kabla ya kuhudhuria

Vijana wamehoji Ofisi ya Msajili kujadili Akidi tu na siyo taratibu za kikatiba na kisheria


Wametuhumu pesa ziliozogawanywa na ushiriki wa kiongozi wa chama cha upinzani


Vijana- NCCR wanahisi Ofisi ya Msajili wa vyama inatumiwa kumtimua Mwenyekiti Mbatia


Jambo la kuzingatia ni kwamba Wajumbe waliokwenda TCD ndicho chanzo cha Mgogoro

Ni kupitia TCD kilipatikana kikosi kazi cha Rais kinachokusanya maoni kuhusu ''Demokrasia ''


Kukosekana kwa CHADEMA na NCCR kunafanya kazi ya kikosi kazi kuwa ngumu kukubalika

Uwepo wa Wajumbe wa NCCR ndani ya TCD ni sawa na ule wa COVID19 ndani ya Bunge


Swali la kufikirisha, kwanini 'Uasi' ndani ya vyama unalindwa kwa kutumia taasisi za serikali?


Mwenyekiti Mbowe ameongoza ujumbe Ikulu kwa kinachoitwa maridhiano ya Kitaifa

Hakuna anayejua nini Mbowe aliongea na Rais SSH mara 2 na ya 3 akiwa na ujumbe


Kuna mgawanyiko ndani ya Chadema kwa mitazamo tofauti katika makundi mawili;


Kundi linaloamini maridhiano yana tija kwa kuzingatia nia ya Mh Rais kuonge na Wapinzani.

Kundi la Pili linasema serikali haijaonyesha nia njema ikiwemo suala la ''Wabunge COVID19'


Si nia ya bandiko hili kueleza nani yupo sahihi au la baina ya makundi hayo, hata hivyo kutoridhiana ni chanzo cha kufarakana kama historia za vyama vya siasa nchini itazingatiwa


Tofauti kimitazamo ni jambo jema, je wote wana uvumilivu wa ''kukubaliana kutokubaliana'?


Chadema kutoshiriki TCD na Kikosi kazi haiwapendezi wanaotaka hayo yafanyike


NCCR wamejaribiwa na Wanachama wao leo kuna mgogoro unarindima ukiwa na mikono!!

NCCR walifuata taratibu za vikao halali, ' mapinduzi ' yakiwa na mikono mingi yanatokea


Kwamba Mapinduzi yanajengewa uhalali kuliko vikao halali vya chama, inafikirisha sana!!


Kwa nama yoyote fursa ikijitokeza kuhujumu Chadema itatumiwa kikamilifu.

Udhamini kwa CODVID19 na ''NCCR waasi'' una nguvu kubwa sana nyuma yake


Chadema watambue wamebeba sura ya 'uasi' na ugumu usio na lazima hasa suala la katiba


Ikiwa kuna fursa ya kuvuruga Chadema, hoja ya Katiba na kutaka ushiriki TCD fursa hiyo itapewa kila msukumo na nguvu yoyote kwa gharama zozote.


Ni ugumu huo ambao Mwenyekiti Mbatia anajaribu kuutafutia dawa lakini naye anatafutiwa


Adui siku zote hushambulia penye udhaifu. Waswahili wanasema kamba hukatikia pabovu

Kwa wakati walio nao Chadema na mikinzano ya mitazamo lazima wachukue tahadhari


COVID19 iwe funzo wanavyokingiwa kifua na mikono mingi yenye nguvu bila kujali sheria


Hakuna wakati Chadema inakuwa ''vulnerable' kwa attack kuliko sasa kwa sababu ni mbili;


1. Inaonkeana kikwazo cha siasa kama chama kikuu cha Upinzani katika TCD na Kikosi kazi

2. Mazungumzo ya Ikulu yanagawa wanachama na kutengeneza fursa ya kuwavuruga mazingira yatakapotengamaa


Tahadhari zote zichukuliwe na tamko la kushikamana NCCR kama kuna harufu za uchafu


Bila tahadhari, ya CUF na sasa NCCR yanaweza kuitokea Chadema!


Neno la leo


 
 
Back
Top Bottom