Jinsi ya kujua uwiano wa uzito na urefu wako kiafya

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Uwiano wa uzito wa mwili kulingana na urefu kitaalamu hujulikana kama BODY MASS INDEX (BMI)


Uwiano huu hupatikana kwa njia ya hisabati ambapo hugawanywa UZITO WA MWILI (KG) kwa kipeo cha pili cha UREFU wa mwili Katika mita


BMI=uzito wa mwili/kipeo cha pili cha urefu


BMI husaidia kujua kama mtu ana uzito wa kawaida, mkubwa, au mdogo


Walio na uzito mdogo wana BMI pungufu ya 18.5 na uzito mkubwa ni 24.9


Uzito wa kawaida lazima uwe na BMI Kati ya (18.5-24.9)


Mtu mwenye BMI chini ya 18.5 kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo KIAFYA vile vile mtu mwenye BMI zaidi ya 24.9 ana matatizo kiafya.


By riba


 
 
Back
Top Bottom