Mradi wa nyumba za kuuza (PSPF, PPF, NSSF) wa Buyuni Dar es Salaam

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Salaam wana JF!

Kuna mradi mkubwa wa kujenga nyumba za kuuza unaoratibiwa na PSPF, PPF nadhani na NSSF uliopo eneo liitwalo Buyuni - Chanika jijini Dar es Salaam. Ninamiliki kiwanja eneo hilo pia na Hati ninayo. Nimefika eneo hilo leo nikakuta nimezungukwa na nyumba zilizokwisha anza kujengwa na hayo mashirika. Niliowakuta eneo hilo kwa leo wakaniambia huwa wanajenga kiwanja chochote kilichowazi/hakijaendelezwa.

Kwa mwenye kufahamu juu ya hili naomba kufahamishwa.

Nawasilisha


 
 
Back
Top Bottom