Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Napendekeza nadharia tete (Hypotheses) zifuatazo, lengo kuu ikiwa ni kutupa sote nafasi ya kuzipima nadharia hizi tete, kwa kutumia uzoefu wetu na uelewa wetu juu ya utamaduni wa CCM, hasa kwa kuzingatia matukio na mazingira ya nyakati hizi. Matokeo ya zoezi hili la kupima nadharia tete hizi yatatoa majibu ya aina mbili: Aidha majibu - KWELI, hivyo kufanya nadharia hizi tete kusimama, au majibu - Siyo KWELI, hivyo kuziangusha hizi nadharia tete. Nadharia tete zipo nne kama ifuatavyo:


I. Ingawa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM halazimiki atoke miongoni mwa wajumbe wa NEC na pia suala hili halipo kikatiba, Chama Cha Mapinduzi hakina utamaduni wa kuteua wagombea wake wa Urais ambao siyo miongoni mwa wajumbe wa NEC.


II. Ili mwana CCM awe na nafasi nzuri ya kuteuliwa kubeba bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, inamlazimu mwanachama huyu, agombee na ashinde uchaguzi wa wajumbe wa NEC kwenye uchaguzi wa ndani wa CCM mwaka huu wa 2012. Kwa kufanya hivyo, mwana CCM huyo atakuwa ni mjumbe wa NEC-CCM ifikapo mwaka wa uchaguzi mkuu, 2015, hivyo kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuteuliwa kubeba bendera ya CCM mwaka 2015.


III. Wanachama wa CCM wenye malengo ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015, ambao kwa sasa wanashikilia nafasi mbili kwa pamoja – yaani ubunge na ujumbe wa NEC, chini ya mabadiliko ya katiba ya CCM ya hivi karibuni, itawalazimu aidha waachie nafasi zao za ubunge na kubakia wajumbe wa NEC, au waendelee na Ubunge na waachane na ujumbe wa NEC, huku wakisubiri Baraka za Mwenyekiti wa CCM Taifa za kuwateua kuwa wajumbe wa NEC, kupitia zile nafasi kumi, miezi michache kabla ya mchakato wa kutafuta mgombea Urais kupitia CCM, ili mwanachama huyo awe katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda katika kinyang’anyiro hicho May, 2015.


IV. Kwa maana hii, Mchezo wote wa kinyang’anyiro cha Urais kupitia CCM mwaka 2015, umebadilika kutokana na mabadiliko ya katiba ya CCM, hivyo tutarajie majina mapya kutawala mbio hizi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa CCM Novemba mwaka huu wa 2012, majina ambayo wengi hatukuyatarajia.


 
 
Back
Top Bottom