Nataka Pesa Zangu Zote wakati wa kustaafu

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Nini kingetokea iwapo kingesikilizwa kilio cha "Nataka Pesa Zangu Zote wakati wa kustaafu"?


Karibu tukokotoe.


Tukubaliane *Dhana* za awali:


*Fungu A.*

Mshahara kwa mwezi wakati wa kustaafu: 1, 000, 000 TZS

Mshahara kwa mwezi muda wote wa utumishi: 1, 000, 000 TZS

Muda wa utumishi: Miaka 20 (miezi 240).

Mtumishi atastaafu kwa lazima.

Mtumishi hataishi kupokea pensheni ya kila mwezi hata ya mwezi mmoja.


*ZINGATIA*; katika hali halisi wengi huanza na mishahara midogo na hupata mishahara iliyoongezeka mwishoni kuliko mwanzoni.


Zingatia pia watumishi wengi hawafariki siku ya kustaafu.


Makato: (i) Asilimia tano kwa mwezi (5%)

(ii) Asilimia kumi kwa mwezi (10%).


*Fungu B.*

Mshahara kwa mwezi wakati wa kustaafu: 1, 000, 000 TZS

Mshahara kwa mwezi muda wote wa utumishi:


Miaka mitano ya kwanza: 400, 000 TZS

Miaka mitano ya pili: 600, 000 TZS

Miaka mitano ya tatu: 780, 000 TZS

Miaka mitano ya mwisho: 1, 000, 000 TZS


Muda wa utumishi: Miaka 20 (miezi 240).


Makato: (i) Asilimia tano kwa mwezi (5%)

(ii) Asilimia kumi kwa mwezi (10%).


Mtumishi atastaafu kwa lazima.

Mtumishi hataishi kupokea pensheni ya kila mwezi hata ya mwezi mmoja.


*MATOKEO:*


*FUNGU A*

Jumla ya Akiba (Michango yako makato 5%) 12, 000, 000.00 TZS


Jumla ya Akiba (Michango yako makato 10%) 24, 000, 000.00 TZS


Hizo ndiyo pesa *ZAKO* ulizoziweka kwenye mfuko wa pensheni. Bila kujumuisha michango ya *MWAJIRI*.


Pensheni ya Jumla: 62, 068, 965.52 TZS


Kiinua Mgongo siku ya kustaafu: 15, 517, 241.38 TZS


Pensheni ya kila mwezi: 310, 344.83 TZS


Pensheni ya Kila Mwezi kwa miaka mitatu: 11, 172, 413.88 TZS


Jumla ya Malipo toka kwa Mfuko: 26, 689, 655.26 TZS


Kiinua Mgongo + PensheniYaMiaka3 – Michango Yako (5%) = 14, 689, 655.26 TZS


Kiinua Mgongo + PensheniYaMiaka3 – Michango Yako (10%) = 2, 689, 655.26 TZS


*TAFSIRI RAHISI*


Kwa utaratibu ulioko sasa,


Wenye makato 5%, kwa Mshahara wa 1, 000, 000 toka kuajiriwa kwa miaka ishirini;


Unalipwa kiinua mgongo 3, 517, 241.38 TZS *ZAIDI* ya michango uliyotoa.


Ukiongezea na pensheni ya miaka 3 watakayolipwa warithi: atakuwa amepokea 14, 689, 655.26 TZS *ZAIDI* ya michango yake aliyotoa.


*FUNGU B*

Jumla ya Akiba (Michango yako makato 5%) 8, 340, 000.00 TZS


Jumla ya Akiba (Michango yako makato 10%) 16, 680, 000.00 TZS


Hizo ndiyo pesa *ZAKO* ulizoziweka kwenye mfuko wa pensheni. Bila kujumuisha michango ya *MWAJIRI*.


Pensheni ya Jumla: 62, 068, 965.52 TZS


Kiinua Mgongo siku ya kustaafu: 15, 517, 241.38 TZS


Pensheni ya kila mwezi: 310, 344.83 TZS


Pensheni ya Kila Mwezi kwa miaka mitatu: 11, 172, 413.88 TZS


Jumla ya Malipo toka kwa Mfuko: 26, 689, 655.26 TZS


Kiinua Mgongo + PensheniYaMiaka3 – Michango Yako (5%) = 18, 349, 655.26 TZS


Kiinua Mgongo + PensheniYaMiaka3 – Michango Yako (10%) = 10, 009, 655.26 TZS


*SOMO*

Endapo kilio cha "nilipwe *HELA ZANGU NILIZOCHANGIA! 1!*" kitasikilizwa, Mtumishi atapokea kiinua mgongo kidogo kuliko anachopokea sasa hivi.


*"Be very careful what you wish for, because you might very well get it"*. ~ Msemo wa Bazungu.


*HINT:* Pakiwa na makosa ya ukokotoaji popote hapo, nijuze.


 
 

Related Discussions

Back
Top Bottom