NMB: Makato mapya kwa wateja wa NMB yaja yakiwa yameongezeka mara mbili zaidi ya sasa?

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Habari


Kama kichwa Cha mada kinavyojieleza ni kwamba tarehe 3/2/2019 Makato mapya kwa watumiaji wa benki ya makabwela yataongezeka Kama nilivyojaribu kudodosa.


Cash withdrawal fees kwa ATM mashine itakuwa ni sh.1150/= kutoka ile ya zamani sh. 940/=

Kutoa pesa kaunta itakuwa ni sh. 6, 500/= kutoka ile ya zamani sh. 4012/=


Kuhamisha fedha kwenda benki nyingine itakuwa ni sh. 2, 000/=


Kuweka hundi kutoka benki nyingine itakuwa ni sh. 1, 000/= ambayo zamani ilikuwa no bure


Kwenye kutoa pesa kwenda kwenye mobile money hela yake ni Mara mbili ya sasa. Kweli uchumi unakua kwa 7.1/%


Ila mnyonge lakini Haki yake mpeni niwapongeze kwamba mmeondoa yafuatayo;


Monthly maintenance fee ilikuwa sh.1, 900/= Sasa itakuwa BURE


Kuhamisha pesa kwa NMB mobile nayo itakuwa bure.


Sasa naona NMB inawahimiza watu mukaweke pesa zenu benki maana hazitakuwa na Makato ila ole wako ujifanye kwenda kuzidraw utafurahi na roho yako.


Kweli uchumi unakuwa tutembee vifua mbele


 
 
Back
Top Bottom