Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Nimeisikiliza wimbo mpya wa Roma mkatoliki Leo

Nimependa pale anaposema ""Mungu wa daudi mungu wa Paulo na mungu wa yohana""""

Hio sentensi hapo naona inamajibu karibu yote ya kutekwa.


Rapa Roma Mkatoliki ameachia video ya wimbo wake ‘Zimbabwe’ ukiwa ni wimbo wake wa kwanza tangu alipotekwa na kuteswa kwa siku tatu.

Kupitia ‘Zimbabwe’ Roma amesimulia tukio la utekaji wake, watu anaoamini walimteka na sababu za kuamua kutoendelea kufuatilia jarada la upelelezi wa tukio hilo.


Mkali huyo pia amezungumzia kitendo cha baadhi ya wasanii wenzake kutomtembelea alipokuwa anauguza majeraha ya mijeredi ya watesi wake.

Pia, rapa huyo amezungumzia kauli ya Mbunge aliyedai bungeni kuwa amemtukana mkuu wa nchi.


Mkali huyo wa mashairi yenye mvuto wa maajabu (Rhymes of Magic Attraction) amekanusha tetesi kuwa watekaji wake walikuja na Noah huku akiwachana kuwa waachane na tabia za kutekana na kutumia silaha bali washindane kwa hoja.





Mashairi ya Wimbo


Wengi mlijiuliza walionteka ni maaskari?

Mkanitafuta vituo vyote central hadi stakishari

Wakasema… hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari

Dah.....

Ya Kaisari mwachie Kaisari

Machozi yenu yatalipwa mimi nafunga na kusali


IMBA ROMA IMBA X3


Mungu wa Paulo… ndiyo Mungu wa daudi

Na ndiyo Mungu wa John mnayemuita Yohana Wayahudi

Mwanangu alimuuliza, mama baba lini atarudi?

Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sinabudi


Fahamu yakuwa..


Me siyo tu rappa pia ni baba wa familia

Na watoto mahitaji nawapa kama isemavyo biblia


Kipi bora?..


Nife museme nilikufa kiharakati?

Siogopi kufa… ila nnawaachaje waliobaki?


Je?..


Nani katiyenu mwanangu atampa malezi?

Wapi atapata mahitaji?

Wapi atapata mapenzi?

Mama naye?..

Wapi atapata mahitaj na malezi?

Na report ya upelelezi

Vipi akiteka mtekaji?


Je?…


Kaburi langu mtalipalilia majani?

Nimeumwa hamjakuja kuniona

Mnangoja mje msibani?

Nlipokuwepo skuwa nnajua hii saa nne hii saa nane

Nlichohitaji… nitoke mzima na ndugu zangu tuonane


Nimechapwa mijeledi

Nimevunjwa bila huruma

Ahsante mliopaza sauti

Nimeiona nguvu ya umma

Siku tatu nimefumbwa macho

Mikono nimefungwa nyuma....


NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMBOBWO YELELE MAMA WEE X4


IMBA ROMA IMBAA... SEMA BABA WEEEE


Nasimama na nnaunga hoja kwenye uchumi wa viwanda

Nanasi linaoza msoga kibiti linaoza shamba

Walioniteka hawakuja na noah… ni uvumi na visanga

Ila KUTEKANATEKANA Ni uhuni wa kishamba…

Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja

Maana sote lengo letu ni kuijenga Tanzania moja

Me skuona nyota kwa shoulder ila najua we ni soja


Inshaalah..


Ulikuja mwenyewe ama ulipewa order?


Ewalah..


Aminini siku hazigandi

We ni yanga me ni samba kuwa mpinzani siyo dhambi

Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani

Samba akichukua kombe sijui atapona nani?


Na kuna Mbunge alisema eti nimemtukana mkuu

Utahukumiwa na mkono wa Mungu… namshtakia aliye juu


Kwanza lini?

Na kwanini?

Me nimtukane mjomba?

Umepewa gari ya wagonjwa mimi Tanga najengewa bomba


Me mbarikiwa na nikifa kuume kwa baba ntaketi

Na mtu wa watu.. That’s why lilisimama bunge la

Bajeti Kunijadili mtanzania kuwa MAKINI PIA MAKINIKIA

NAYATUNGIA MAPINI PIA


Me nlitabiri utakuwa rais kipindi unaitwa waziri

Japo maisha siyo rahisi ila pongezi unastahili

Waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili

God bless imetimia injili niliyoitabiri


NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMBOBWO YELELE MAMA WEE X4


IMBA ROMA IMBAA

SEMA BABA WEEEE


 
 
Back
Top Bottom