Uza kitabu chako/nunua kitabu kwa app ya Vitabu (Google Playstore)

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Vitabu App ni application maalum ya simu ambayo itatumika kama sehemu ya

Kuuzia vitabu ya aina mbalimbali. Ni app iliyo chini ya kampuni ya Mindtap

Tanzania Limited inayomilikiwa na Watanzania.


App hii imetengenezwamahsusi kama njia mbadala ya wachapishaji wa vitabu na waandishi kuuzakazi zao kwa watumiaji wa simu Tanzania na nchi zingine duniani.

Inafahamika kuwa Tanzania hakuna platform thabiti ya uuzaji wa vitabu kwa

Mfumo wa djitali kama ilivyo Kindle Amazon ambayo kwa bahati mbaya

Haipokei kazi za Kiswahili.


Hivyo, wachapishaji na waandishi wameendelea kutegemea mfumo mmoja tu wa

Vitabu vilivyochapishwa. Katika nyakati hizi ambapo matumizi ya

Smartphones na internet yameongezeka kwa kiasi kikubwa hapa nchini, kuna

Fursa kubwa wachapishaji kama Mkuki na Nyota kuweza kuwafikia wateja

Wengine wengi zaidi.


INAVYOFANYA KAZI


Vitabu vitawekwa kwenye application kwa mfumo wa PDF. Msomaji atapewa

Kurasa chache za mwanzo (walau 10 – 15) kwa ajili ya preview ambayo ni

Bure. Anapotaka kununua kitabu, atalipa kwa njia ya M-Pesa, Tigo Pesa na

Airtel Money. Atatumiwa token maalum kwa ajili ya kutumia kudownload

Kitabu. Kitabu kitahifadhiwa kwenye maktaba ya kwenye simu ambacho

Atakisoma katika muda wowote anaotaka kwa urahisi na muonekano bora.


USALAMA


Vitabu hivi vitawezwa kusomwa kwenye app hiyo pekee. Hakuna uwezekano wa

Mtu mmoja kumtumia mtu mwingine (no sharing). Maana yake ni kwamba mtu

Anaponunua kitabu kwenye app, ni sawa na yule anayenunua kitabu cha

Kawaida. Pia kwa mwenye simu, pale anapopoteza simu au kuiformat, vitabu

Vyake alivyonunua vitarejea kwenye maktaba yake.


UKAGUZI NA USIMAMIAJI WA UNUNUZI


Mchapishaji atapewa akaunti maalum ambayo ataweza kukagua kila hatua ya

Manunuzi yanayofanyika ya vitabu vyake. Hiyo itampa access ya moja kwa

Moja kufuatilia mauzo yake. Biashara itakuwa ya uwazi wa hali ya juu.


WATU WA NCHI ZINGINE WANAWEZA KUNUNUA?


Kwa sasa, wasomaji wa Kenya wanaweza kununua vitabu kwenye app kwa kutumia

M-Pesa. Zambia na UGANDA wataweza kununua kwa kutumia mtandao wa MTN. Baadaye

Tunafanya utaratibu malipo yaweze kufanyika dunia nzima.


Kama una kitabu na unapenda kukiuza, tafadhali piga simu 0766173514. Email, Vitabu@mindtaptz. Com


 
 
Back
Top Bottom