Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Baada ya siku nyingi kupita leo nimemkumbuka rafiki yangu kipenzi ambaye alipatwa na matatizo makubwa katika safari yake yakusaka maisha miaka kama 5 iliyopita tukiwa kidato cha sita yaani kila nikikumbuka nabaki kulia tu.


Wakati naripoti shuleni nilikuwa nimechelewa kidogo baada ya kufika pale kutokana na jitihada zangu za masomo darasani nilitokea kuelewana na jamaa mmoja alikuwa anaitwa Agustino yeye alikuwa anasoma HGE mimi nilikuwa EGM masomo mengi tulikuwa tunaendana tukawa tunadiscuss pamoja


Kumbe jamaa huyo Agustino alikuwa amejisajili kama Private Candidate so alikuwa anatokea kitaa kuja shuleni baada ya urafiki kuzidi nikawa natoroka mara kwa mara tunaenda kukaa getto na kupiga story pamoja na masela wengine


Kifupi wakati ule nilikuwa na kama miaka 18 lakini kutokana na mwili wangu tulikuwa tukitembea nae unaona kama mimi nimkubwa maana alikuwa anamwili mdogo mdogo sana


Wakati natoka nyumbani nilikuwa bado sina mawazo kichwani ya kuwa na pesa nyingi nilichokuwa naona mbele yangu ni namna gani nitafaulu kidato cha sita michongo ya pesa niliowahi kufanya ilikuwa ni vibarua vya kawaida kitaa


Lakini jamaa yangu alikuwa ni mtu wa mishe mishe nyingi kila akikaa lazima apigiwe simu, tukiwa tunaongea lazima apige story za maswala ya pesa. Wallet yake akitoa hela unaona imejaa misimbazi nikawa najiuliza jamaa hizi hela anatoa wapi nikabaki kusema labda kwao watakuwa wanajiweza sana, japo ukimuangalia vizuri haonekani kama katokea kwenye rich family.


Getto alipokuwa amepanga lilikuwa limesheheni kila kitu,

Mtaani pale alikuwa amezoeleka na watu wengi chocho nyingi akawa ananionyesha sasa kuna siku weekend kaniambia nimsindikize akachukue pesa yake kwa jamaa yake mmoja.


Alinipitia pale shuleni tukaondoka kuelekea kwa huyo jamaa shule tuliokuwa tunasoma iko maeneo ya kijijini so tulukuwa tunapita njia za vichakani chakani kuna mashamba wanalima nyanya, na matikiti maji nyumba ziko mbali mbali sana.


Baada ya kuvuka kamto tufika kwa yule jamaa mimi ikabidi ni baki njee halafu jamaa mwenyewe kumuona umri ulikuwa kama umeenda hivi, alikuwa na zaidi ya 50 year tulisalimiana wenyewe wakaingia ndani lakini kwa njee nilisikia kama mabishano ambayo sikujua wanazungumzia nini....


Kwa mwendelezo bonyeza link hizi.


Sehemu ya pili

Sehemu ya tatu


Sehemu ya nne

Sehemu ya tano


Sehemu ya sita

Sehemu ya saba


Sehemu ya nane

Sehemu ya tisa


Sehemu ya kumi

Sehemu ya kumi na moja


Sehemu ya kumi na mbili

Sehemu ya kumi na tatu


Sehemu ya kumi na nne

Sehemu ya kumi na tano


Sehemu ya kumi na sita

Sehemu ya kumi na saba


 

Original publication date: 2026-09-05
 
Back
Top Bottom