- Joined
- Mar 14, 2026
- Messages
- 33,422
Katika kuangaza macho kwenye media nilikutana na hotuba/mahojiano ya Nyerere na akakiri kwamba wao kama wapigania uhuru hawakuwahi kuleta jambo jipya liwalo lolote katika nchi hii.
Kama ni mipaka waliikuta. Kama ni jina la nchi walilikuta, kama ni taifa walilikuta, kama ni watu waliwakuta. Nyerere anakiri wazi kuwa jambo pekee walilofanikisha wao ni kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar. Hii yaweza kuwa kigezo cha kuutetea Muungano?
Viongozi wa sasa hawampendi Mwalimu, lakini wanajaribu kutetea Muungano kwa kadri wawezavyo. Najiuliza, ili kufanya kitu kipya nje ya wakoloni ilikuwa ni lazima kufanya Muungano? Ambapo Muungano wenyewe una nyufa na viraka hadi basi.
Leo Muungano ukifa, sisi kama Taifa tutakuwa na lipi la kujivunia?