Faida/Changamoto za biashara ya Mabasi

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Wakuu


Kuna kitu hapa natamani tujaribu kujadiliana kwa pamoja juu ya hii biashara ambayo imeonekana kuacha watu wengi na maswali huku watu wengi pia wakiwa na majibu.


Tujadiliane kuhusu biashara hii ya mabus makubwa Engine Model za Scania, Yutong, Nissan, Diesel, Zhongtong Higer, Kinglong, nakadhalika.


Mimi kwa upande wangu biashara ya mabusi ndiyo biashara pekee ya ndoto zangu. Pamekuwa na kauli nyingi za ukweli na pia zipo za kupotosha, wapo wanaoamini huwezi kufanya biashara ya mabusi bila kuwa mshirikina wapo pia wanaoamini wamiliki wa mabusi wanapata faida maradufu.


Jamiiforums ina bahati kunipata mimi atleast wanajamiiforums wataweza kupata baadhi ya majibu wanayojiuliza kuhusu biashara hii, nasema baadhi ya majibu kwa sababu si kila kitu kinafaa kuweka hadharani. Uchawi ndiyo neno kuu linalotawala mtu anapozungumzia biashara hii.


Je, wapigadebe wananafasi gani kwenye biashara hii. Je, ni kweli bank zinaongoza kukopesha wamiliki wamabusi


NB: Watu wenye nyota zenye asili ya moto au chuma wanaweza kufanya biashara hii na kufanikiwa


Je, wewe unafahamu nini kuhusu biashara hii?


----------------------


Baadhi ya michango


 
 
Back
Top Bottom