Jk kumuita daimond ikulu kumjulisha shoo ya us imekaaje???????

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422



Stori: Sifael Paula; www.globalpublisherstz.info


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz' na kumpa jukumu maalum, Ijumaa linairusha hewani.

Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti' alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni.

"Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani.

"Kwa mara ya kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja. Sasa hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari," alisema Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye mchongo huo hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo na mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins.


 
 
Back
Top Bottom