Kwa wanaoifahamu Zambia; Msaada tafadhali nahitaji kwenda kufanya biashara huko

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Heshima kwenu Mabibi na Mabwana.

Mimi nilishakaa pale boda ya Tanzania na Zambia kwa miezi kadhaa kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali, na katika kuwa kwangu pale kuna mtu nilikutana nae na akanambia kule Zambia kuna fursa nyingi tu za biashara kwa kuwa bidhaa nyingi za Zambia zinatokea Tanzania japo hakunielezea kwa undani ila alinambia bidhaa km mafuta, unga, sabuni zinaenda sana kule

Sasa kama kuna mwenye taarifa za kutosha na jinsi ya kupeleka biashara na kupata fursa uko Zambia atuekee hapa ili tupate pa kuanzia,

Mchango wako ni muhimu sana mana ajira imekua zoezi

Natanguliza shukrani Wakuu.


 
 
Back
Top Bottom