Mabati ya Kiboko G28 yana matatizo, TBS mko wapi?

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Nimenunua mabati ya kiboko G28 lakini wakati wa kuezeka fundi akanieleza kuwa hayakai kwenye usawa kama ailvyozoea.

Nilipoyapima nikapata vipimo vifuatavyo

Upana: sehemu ya chini ni cm 82 na sehemu ya juu ni cm 86

Diagnal: moja ni cm 310 na nyingine ni cm 312

Kwa mshangao mkubwa mabati haya yana nembo ya TBS.

Je nifanyeje? TBS mnakagua kiwanda hiki?


 
 
Back
Top Bottom