Wenye taarifa za fursa za kibiashara popote Africa

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Habari wanajamvi wote.


Kuna mada mbalimbali za fursa za kibiashara zilizowekwa hapa jf hasa za Uganda, China, Thailand na Turkey.


Nimetumia taarifa hizi nimefika Uganda na najipanga kukua zaidi nifike hadi huko China au Thailand na Turkey kibiashara.. Lakini kabla ya kufika huko inawezekana hapa hapa Africa kuna uwezekano wa kufanya biashara nzuri kabisa...


Najua umaskini wetu ni kukusa taarifa sahihi, na hapa ni makutano ya njia panda ambapo watu wengi tofauti wana taaarifa za kutosha kutoka maeneo mbalimbali hapa Africa kama Zimbabwe, Botswana, Mauritius, Lusaka nk.. Naamini kote huku kuna Watanzania walioona fursa huko na kuweza kuzimwaga hapa kama wanavyofanya wakina Money Stunna luck saba saba n. K.


Tiririkeni kuonesha fursa zilizopo huko, na aina ya fursa, currency yao, gharama za hotel na eneo zuri kwa mgeni kulala kwa bei ndogo na wapi pa kupata bidhaa au fursa za maeneo hayo...


 
 
Back
Top Bottom