Nataka nikope Tsh milioni 10 SACCOS ninunue gari. Niambie uzoefu wako ulivyokopa pesa na kununua gari

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Wakuu mimi ni kijana tu under 35 yrs old kwa ajira yangu niliyobahatika nayo napata 1mil as take home, natamani sana kuwa na kigari changu cha familia maana nikipiga hesabu za elf 10 kila siku.


Za mishe za kuwapeleka outing wife na watoto wangu napoteza pesa nyingi sana mambo ya nauli ya Bolt, kwa sasa sina keshi ya kusema nitachukua ya kwangu kama 10 mil hapana ila kwenye kukopa hesabu zinakubali na kwa saving yangu kupata keshi yangu kama yangu itabidi kusubiri mitano tena.


Naombeni mnipe changamoto zitakazojitokeza baada ya kununua gari la mkopo hapo ukizingatia bado nimepanga, sijui kuendesha gari, sina leseni.


Thanks.


 
 
Back
Top Bottom