Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Wakuu habar, nimewaita hapa, tupeane mbinu za biashara na changamoto zake, mbinu zangu mimi ni zifuatazo, huwa natumia mbinu ya kumwambia dereva kuwa ukileta hesabu wiki nzima, wiki inayofuata nampunguzia hesabu, badala ya 7000, namwambia alete 6000, hapo akirin nimepiga hesabu kuwa nimemuachia hesabu ya siku moja kama offer, na hapo biashara inaenda vizuri sana. Njia nyingine, nawaambi kila tarehe 15 hutakiwi kuleta hesabu, na kila tarehe 30 utakiwi kuleta hesabu, na achukue yeye hizo pesa, lakini sharti langu siku zote lazima ulete hesabu kamili, ili uweze kupata offer hiyo. Nawaombeni na nyinyi wenzangu mtoe mbinu zenu, ili tufanikiwe na hizi biashara.


 
 
Back
Top Bottom