- Joined
- Mar 14, 2026
- Messages
- 33,422
Salama wana JF. Ninategemea kuingia katika biashara ya kuleta mashudu ya pamba (cotton cake) toka kanda ya ziwa, kwa wale wanaotengeneza vyakula vya mifugo. Ilikujua ni kiasi gani niwe naleta nahitaji msaada wa JF. Naomba kwa wale wanaohitaji/watakaohitaji wanijuze ili nimalizie buss plan. Au kwa mwenye ushauri wowote juu ya soko la cotton cake/shudu la pamba pia karibu sana. Asanteni sana