Nataka kuanza hii biashara japo wengi mtanishangaa, naomba uzoefu wenu

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Habarini wanajamvi, mimi ni muajiriwa wa private sector. Sasa kama mnavyojua jamani maisha ni kujitafutia mbali na kauajiriwa.


Kwa upande wangu baada ya kukaa kwenye ajira kwa miaka mitatu nimeona ni wakati muafaka wa kufanya side hustle itakayoniongezea kipato.


Sasa baada ya kufikiria sana kuhusu wazo la biashara ikiwa ni pamoja na kupita mitandaoni, nikapata idea ya kuuza SEX TOYS. Nafikiri wengi tunaelewana, maana yake nataka nianze kuuza penis na vagina za bandia kupitia mtandao au niseme Instagram.


Wazo hili nililipata baada ya kuona page fulani huko Instagram inayojihusisha na biashara hii. Japo si biashara ambayo kwa macho ya kawaida unaweza ukaifanya ukiwa open kabisa. Lakini kwa maisha ya sasa nimeona kama inaweza ikafaa na ikanipa faida bila kujiexpose sana.


Sasa shida inakuja sijajua kwa hapa bongo hivi vitu vinapatikana wapi kwa kuanzia. Maana nilikuwa na wazo la kuagiza kutoka nje lakini kabla sijafika huko nianze na hapa home.

Sasa ndugu zangu wale ambao mnaweza mkanipa idea ya namna ya kupata hizi bidhaa kwa bei ya jumla na mimi nikaanza taratibu kabla sijaanza kuagiza kutoka nje.

. Sana sana nipate chimbo la hapa home kwetu, kama ni dar vinapatikana wapi na wapi na nawezaje kuwapata hao wauzaji.


Karibuni wajumbe, leo tudiscus kitu kipya kabisa. Maana sijaona humu ndani watu wakizungumzia hii biashara.


 
 
Back
Top Bottom